YESU ANAKUJA NITAKWENDA. MKUTANO MKUU NTUC 2025

7-9 SEPTEMBA 2025. UNIVERSITY OF ARUSHA

Salamu katika jina la Mwokozi wetu anayekuja upesi, Yesu Kristo!
Kwa furaha na shukrani kubwa, ninakukaribisheni kwenye Mkutano wa 4 wa Union ya Kaskazini mwa Tanzania wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, unaofanyika hapa Chuo Kikuu cha Arusha kuanzia Septemba 07-09, 2025.
Kaulimbiu ya Mkutano huu, “Yesu Anakuja, Nitakwenda!”, inatuita sote kuthibitisha upya tumaini letu katika kurejea kwa Bwana wetu na kuhuisha tena shauku yetu ya kuitikia wito Wake—kwenda popote anapotuongoza, tukishiriki injili ya milele kwa ulimwengu.
Mkutano huu siyo tu muda wa kutekeleza kazi muhimu ya utendaji wa kanisa katika eneo la Kaskazini mwa Tanzania, bali pia ni fursa ya baraka kwa ajili ya ushirika, ibada, msukumo wa kiroho, na uamsho. Sisi kama wajumbe, waumini, na viongozi, tunakutana kwa umoja ili kutafuta mwongozo wa Mungu, kutathmini maendeleo ya utume wetu, na kufanya maamuzi yatakayoongozwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya mustakabali wa kazi ya kanisa katika eneo letu.
Katika kipindi cha siku hizi mbili, tutashuhudia ibada zenye kuinua mioyo, taarifa za kutia moyo, mipango ya kimkakati, na mashauriano ya maombi. Pamoja tutasherehekea yale Mungu aliyoyafanya, tutakabiliana na changamoto zilizopo, na kukumbatia nafasi mpya za utume.
Tunapoanza Mkutano huu, ninawaalika kila mmoja kuungana nami katika kuomba kwa bidii umwagiko wa Roho Mtakatifu. Tujitafutie uamsho wa kiroho binafsi na wa pamoja, na tujikabidhi upya kwa utume uliopewa kupitia ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6–12 na mwito wa Ufunuo 18:1–4. Ujumbe huu ni wa dharura zaidi leo kuliko wakati mwingine wowote katika historia.
Tunasimama juu ya ahadi kwamba “Hatuna kitu cha kuogopa kuhusu yajayo, ila tu tukisahau jinsi Bwana alivyotuongoza, na mafundisho Yake katika historia yetu iliyopita” (Ushuhuda kwa Kanisa, juzuu ya 9, uk. 10). Hebu tusonge mbele pamoja, kwa ujasiri, mshikamano, na imani, tukitangaza kwa uthabiti: “Ndiyo Bwana, NITAKWENDA!”
Kwa niaba ya Union ya Kaskazini mwa Tanzania, nawakaribisha kwa moyo mkunjufu wajumbe wote na wageni katika Mkutano huu muhimu. Iwe ni wakati wa kumtukuza Mungu, kuimarisha Kanisa Lake, na kuharakisha kurejea kwa Mwokozi wetu.
Mch. Mark Walwa Malekana– Mwenyekiti wa Union ya Kaskazini mwa Tanzania

MCH: MARK W. MALEKANA-MWENYEKITI MSTAAFU WA UNION YA KASKAZINI MWA TANZANIA

 
 
 
 
 
 
 

“Tunapokutana katika Mkutano wa 4 wa Union ya Kaskazini mwa Tanzania, tukumbuke kuwa utume wetu si wa kiutawala pekee bali ni wa kiroho. Kila taarifa, kila mpango, na kila uamuzi tunaoufanya unapaswa kutuelekeza tena kwenye agizo kuu la Kristo—kutangaza injili ya milele kwa watu wote. Mkutano huu na utahuisha umoja wetu, utaimarisha kujitoa kwetu, na kutukumbusha kwamba kwa hakika, Yesu Anakuja, Twendeni!

Mch: Magulilo Mwakalonge Katibu Mkuu Mtaafu, Union ya Kaskazini mwa Tanzania

“Fedha zote tunazokusanya katika kanisa letu zina kusudi moja kuu—utume. Tunaposhiriki kwa uaminifu katika zaka na sadaka, tunashirikiana na Mungu kupeleka injili ya milele kwa ulimwengu. Hata katikati ya changamoto za kifedha na madeni, tumeshuhudia mkono wa Mungu ukituongoza na kutupa ushindi. Hebu tuendelee kusimama pamoja, tukisema kwa imani: Yesu Anakuja, Nitakwenda!

Elder: Mathias Mavanza- Mhazini Mkuu Union ya Kakazini mwa Tanzania

PAKUA APPLICATION MAALUM YA SESSION KUPITIA